Pata taarifa kuu
BENIN-BURKINA FASO-UFARANSA-UGAIDI-WATALII

Benin yachunguza namna watalii wawili wa Ufaransa walivyotekwa

Serikali ya Benin imesema imeanza kuchunguza kutekwa kwa watalii wawili, raia wa Ufaransa waliotekwa na watu wenye silaha tarehe 1 mwezi wa Mei na kupelekwa nchini Burkina Faso.

Rais wa Uafransa Emmanuel Macron akiongoza mazishi ya wanajeshi wawili wa nchi hiyo waliouawa nchini Burkina Faso wakati wakiwaokoa watalii nchini Burkina Faso
Rais wa Uafransa Emmanuel Macron akiongoza mazishi ya wanajeshi wawili wa nchi hiyo waliouawa nchini Burkina Faso wakati wakiwaokoa watalii nchini Burkina Faso Tesson/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutekwa, watalii hao Patrick Picque na Laurent Lassimouillas waliokolewa baada ya operesheni kuongozwa na wanajeshi wa Ufaransa.

Operesheni hiyo ilisababisha wanajeshi wawili kupoteza maisha.

Siku ya Jumanne, rais Emmanuel Macron aliongoza mazishi ya wanajeshi hao wawili na kuwaita mashujaa wa taifa hilo.

“ Cédric de Pierrepont naye Alain Bertoncello, wamekufa ni wazi kuwa kazi iliyofanyika ilipata mafanikio makubwa, lakini ona tumewapoteza wanajeshi wetu wawili, nao wamekufa kama mashujaa kwa ajili ya taifa la Ufaransa,” alisema rais Macron.

“Wamekufa kama mashujaa kwa sababu waliona hakuna kilicho na  thamani kubwa kuliko maisha ya wananchi waliokuwa wametekwa,” aliongeza.

Nchi ya Burkina Faso imeendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama, kutokana na kuwepo kwa makundi yenye silaha ambayo yameendelea kupambana na vikosi vya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.