Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-BENIN-USALAMA

Burkina Faso: mateka wanne waachiliwa, askari wawili wa Ufaransa wauawa

Mateka wawili wa Ufaransa, raia mmoja wa Marekani na raia mmoja wa Korea Kusini wameachiliwa baada ya vikosi vya Ufaransa kuendesha operesheni kabambe kaskazini mwa Burkina Faso.

Hifadhi ya Taifa ya Pendjari, Benin. (Picha ya kumbukumbu)
Hifadhi ya Taifa ya Pendjari, Benin. (Picha ya kumbukumbu) © STEFAN HEUNIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa operesheni hiyo askari wawili wameuawa, ikulu ya Elysee imesema. Mateka hao wawili wa Ufaransa walitekwa mnamo Mei 1 mwaka huu katika Hifadhi ya Taifa ya Pendjari kaskazini mwa Benin ambako walikuwa wakisafari.

Katika taarifa yake, ikulu ya Elysee imetangaza kwamba watalii hao wawili wa Ufaransa walitekwa nyara Jumatano wiki iliyopita kaskazini mwa Benin, katika Hifadhi ya Taifa ya Pendjari, kwenye mpaka na Burkina Faso ambapo kunaripotiwa makundi kadhaa ya wanamgambo wa kjihadi.

Mwanamke mmoja kutoka Marekani na mwengine kutoka Korea Kaskazini pia wameokolewa katika peresheni hiyo ya vikosi vya jeshi la Ufaransa, Elysee imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.