Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UCHAGUZI-SIASA

Chama cha ANC chaongoza katika Uchaguzi Mkuu Afrika Kusini

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), kinaongoza katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano wiki hii, kulingana na matokeo ya awali ya uchaguzi. Tume ya Uchaguzi nchini Afrika kusini imebaini kwamba tayari imehesabu kura kutoka robo ya wilaya zinazounda nchi hiyo.

Vituo vya kupigia kura vikifunguliwa katika shule ya Durban, baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini.
Vituo vya kupigia kura vikifunguliwa katika shule ya Durban, baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Chama cha ANC kinatawala Afrika kusini tangu mwaka 1994.

Chama hiki cha kihistoria cha Nelson Mandela ambacho kina viti vingi bungeni, kinaongozwa kwa 54.65% ya kura, kulingana na takwimu hizo.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA),kinachukuwa nafasi ya pili kwa 26.49% ya kura, kikishinda kabisa chama cha tatu kwa wafuasi wengi nchini cha EFF cha Julius Malema kwa 8.07% ya kura.

Chama cha ANC ambacho kimeendelea kupata ushindi katika chaguzi zotebaada ya kuanguka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi na kuja kwa demokrasia mwaka 1994, kimepoteza umaarufu wake kutokana na kashfa za rushwa zinazoendelea kukabili aliye kuwa rais nchi hiyo Jacob Zuma (2009-2018).

Lakini mrithi wake Cyril Ramaphosa, rais wa sasa wa Afriak Kusini, aliahidi kuimarisha chama na kupambana dhidi ya rushwa, ukosefu wa ajira na tofauti za kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.