Pata taarifa kuu

Uchaguzi Afrika Kusini: ANC yapewa nafasi kubwa ya kushinda

Wapiga kura nchini Afrika kusini wanapiga kura leo Jumatano Mei 8 kuwachaguwa wabunge na maseneta na wakuu wa mikoa. Rais atachaguliwa na Bunge.

Kituo cha kupigia kura cha Cape Town kwa Uchaguzi Mkuu wa Mei 8, 2019.
Kituo cha kupigia kura cha Cape Town kwa Uchaguzi Mkuu wa Mei 8, 2019. © REUTERS/Sumaya Hisham
Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa Afrika kusini wanashiriki katika uchaguzi ambao unafanyika tena miaka 25 tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi na huenda ukawa na changamoto kubwa kwa chama cha rais wa zamani Nelson Mandela Madiba, African National congress (ANC) ambacho kinaendelea kusalia marakani.

Chama cha ANC kinatarajiwa kupata viti vingi bungeni, na kumteua rais Cyril Ramaphosa kuendelea kushikilia uongozi wa nchi.

Hata hivyo chama hiki kongwe cha ukombozi barani Afrika kinaendelea kupoteza umaarufu wake.

Tangu alipochukua hatamu ya uongozi wa chama cha ANC mwaka mmoja uliopita, Cyril Ramaphosa amekuwa akisema kuwa yeye ni mtu wa mabadiliko, atafufua uchumi.

Ramaphosa anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa washirika wa Jacob Zuma ndani ya ANC - na wapiga kura wamechoshwa na kashfa za ufisadi, kukua pole pole kwa uchumi , ukosefu wakazi ambao sasa umefikia 27% na visa vya mara kwa mara vya kupotea kwa nguvu za umeme.

Hata hivyo, Bwana Ramaphosa, ambae anatajwa na jarida la uchumi la Forbes kuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa mwaka 2014 aliamua kuachana na biashara baada ya kuchaguliwa kuwa makamu wa rais.

Gazeti la kifedha la kimataifa la Forbes, lilimnukuu kwamba, "aliachana na shughuli zake za biashara ili kuepuka migogoro ya riba" baada ya kuwa Naibu wa rais wa Afrika Kusini mwaka 2014.

Chama tawala nchini humo, Africa National Congress (ANC) ndicho kilipambana dhidi ya utawala wa kibaguzi chini ya uongozi wa Nelson Madela. Kutokana na hilo, kinaungwa mkono zaidi na watu weusi.

Chama Kikuu cha upinzani, Democratic Alliance (DA) kinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wazungu ambao ni raia wa nchi hiyo.

DA hata hivyo kipo chini ya kiongozi kijana mwenye miaka 38, tena kwa rangi ni mweusi. Si mwengine, ni Mmusi Maimane.

Maimane alijiunga na siasa kupitia chama cha DA mwaka 2011, na baada ya miaka minne, akaukwaa uongozi mkuu wa chama hicho.

Hata hivyo Mmusi Maimane, ambaye ni mweusi, wakosoaji wake wanamwita 'Kibaraka wa Wazungu'.

Naye Julius Malema, kiongozi wa chama cha pili kwa ukubwa cha upinzani Afrika kusini mwenye umri wa miaka 38, anatazawa kama mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa nchini Afrika Kusini.

anaongoza chama cha Economic Freedom Fighters (EFF). Alitimuliwa kutoka chama tawala cha ANC mnamo 2012.

Malema, au "Juju" kama anavyoitwa wakati mwingine amekiweka EFF katika nafasi ya kuwa mrithi wa ajenda kali ya ANC na amefichua mapengo ya chama hicho tawala.

Chama cha EFF kilijinyakulia 6% pekee ya kura zilizopigwa mnamo 2014 katika awamu ya kwanza ya uchaguzi mkuu, lakini ushawishi wake unaonekana kuzidi nguvu takwimu hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.