Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA-AJALI

Ajali ya lori ya mafuta yasababisha vifo vya watu hamsini na tano Niamey

Mlipuko wa lori ya mafuta umeua watu hamsini na tano na kuwajeruhi wengine zaidi ya thelathini, mita chache kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Niger ameliambia shirika la habari la AFP."

Lori la mafuta lililolipuka karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey, Mei 6, 2019.
Lori la mafuta lililolipuka karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey, Mei 6, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii karibu na mji mkuu wa Niger, Niamey.

Idadi ya watu waliofariki dunia ni55 na 36 walijeruhiwa. Wathirika waliteketea kwa moto," ameongeza msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Kwa mujibu wa mashahidi waliohojiwa na shirika la habari la AFP, lori lililokuwa limesheheni mafuta lilianguka kwenye barabara ya reli, nje ya mji wa Niamey. Watu walikuwa wakijaribu kuchota petroli iliyokuwa ikimwagika kutoka kwenye tenki ya lori hilo wakati mlipuko ulipotokea.

"Ilikuwa usiku karibu wa manane wakati nilipotoka na kuona lori limeanguka. Watu walikuja kutoka maeneo mbalimbali kuja kuchota petroli. Kisha nikaona moto upande moja na muda si mrefu nikasikia mlipuko ", mwanafunzi mmoja wa ameliambia shirika la habari la AFP.

Nyumba zilizo karibu na eneo la tukio ziliharibika vibaya.

Hata hivyo shughuli kwenye uwanja wa ndege zimeendelea kama kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.