Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Maambukizi ya Ebola yaongezeka Mashariki mwa DRC

Watu 26 wamethibitishwa kufa ndani ya siku moja kwenye jimbo la Kivu Kaskazini kutokana na maradhi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea, kusumbua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wafanyakazi wa kituo cha kutoa matibabo kwa wagonjwa wa Ebola katika Wilaya ya Butembo wanashughulikia mwanamke aliyambukizwa virusi vya Ebola Machi 28, 2019.
Wafanyakazi wa kituo cha kutoa matibabo kwa wagonjwa wa Ebola katika Wilaya ya Butembo wanashughulikia mwanamke aliyambukizwa virusi vya Ebola Machi 28, 2019. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko wa sasa ni wa pili mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa baada ya ule uliokumba maeneo ya Afrika Magharibi mwaka 2014-2016 na kuua watu zaidi ya elfu 11.

Wizara ya afya nchini DRC imethibitisha vifo vya watu 957, huku ikirekodi visa vya watu 891 ambao wana maambukizi ya ugonjwa huo.

Serikali imetangaza mikakati zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa maambukizi zaidi.

Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola Mashariki mwa DRC yameendelea kuwa magumu kutokana na makundi ya waasi kushambulia vituo vya afya vinavyotoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola.

Kituo kinachotoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wa  Ebola kilichoshambuliwa Katwa, Februari 25, 2019.
Kituo kinachotoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wa Ebola kilichoshambuliwa Katwa, Februari 25, 2019. Laurie Bonnaud/MSF/Handout
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.