Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UN-SAHARA MAGHARIBI

Afrika Kusini yakashifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Nchi ya Afrika Kusini hapo imekashifu vikali hatua ya baraza la usalama la umoja wa Mataifa, lililopitisha azimio kuhusu eneo la Sahara Magharibi, Afrika Kusini inasema azimio hilo ni la upande mmoja.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, serikali yake imekosoa vikali umoja wa mataifa
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, serikali yake imekosoa vikali umoja wa mataifa REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo lililowasilishwa na Marekani, linaongeza muda wa uwepo wa waangalizi kwenye eneo la Sahara Magharibi ambapo lilipata kura 13 kati ya 15 za nchi wanachama huku Afrika kusini na Urusi zenyewe zikijiweka kando.

Balozi wa Afrika Kusini kwenye umoja wa Mataifa Jerry Matjila, aliliambia baraza la usalama kuwa nchi yake inapinga azimio hilo la kuongeza muda wa tume ya MINURSO hadi Desemba 31 na kutoa wito wa mazungumzo kumaliza mzozo uliopo.

Afrika Kusini inasema kwa namna azimio hilo lilivyotengenezwa, limeegemea upande mmoja.

Nchi ya Afrika Kusini imekuwa ikiliunga mkono vuguvugu la Polisario Front linalotaka kujitenga kwa eneo hilo na Moroko.

Umoja wa Afrika unalitambua eneo la Sahara Magharibi kama taifa huru huku pia Moroko ambayo inakalia eneo hilo kwa nguvu ikiwa ni mwanachama wa umoja huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.