Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Tofauti zaibuka kati ya utawala wa kijeshi na viongozi wa maandamano Sudani

Watawala wa kijeshi pamoja na viongozi wa waandamanaji wametofautiana kuhusu muundo wa baraza la pamoja, hali inayoashiria kuwa bado pande hizo mbili licha ya makubaliano ya mwishoni mwa juma, wanatofautiana pakubwa.

Waandamanaji wakionyesha ishara ya ushindi mbele ya makao makuu ya jeshi, Khartoum, Sudan, Aprili 15, 2019.
Waandamanaji wakionyesha ishara ya ushindi mbele ya makao makuu ya jeshi, Khartoum, Sudan, Aprili 15, 2019. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya Jumatatu wiki hii kati ya wanajeshi na wawakilishi wa waandamanaji, yalifanyika baada ya Jumamosi iliyopita kukubaliana kuundwa kwa baraza la pamoja.

Baraza la kijeshi kupitia msemaji wake Luteni Jenerali Shamseddine Kabbashi, limependekeza baraza la watu 10, ambapo wanajeshi watakuwa 7 na raia watakuwa watatu, pendekezo ambalo limepingwa vikali na waandamanaji.

Awali viongozi wa waandamanaji hao walipendekeza baraza la watu 15 ambalo lingejumuisha raia 8 na wanajeshi 7.

Licha ya mazungumzo ya hapo jana kumalizika bila muafaka, viongozi hao wamekubaliana kukutana tena leo Jumanne, huku kila upande ukiwa umefikiria mapendekezo ya kila mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.