Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Martin Fayulu awataka raia kumshinikiza Tshisekedi kuachia ngazi

Kinara wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Martin Fayulu ambaye anadai alinyang’anywa ushindi katika uchaguzi mkuu uliopita, ametoa wito kwa raia kushinikiza rais Felix Tshisekedi aondoke madarakani.

Martin Fayulu, akiwa Brussels, Machi 9 2019.
Martin Fayulu, akiwa Brussels, Machi 9 2019. © NICOLAS MAETERLINCK / BELGA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mbele ya wafuasi wake waliojitokeza kumpokea jijini Kinshasa, Fayulu ametolea mfano maandamano ya raia kwenye nchi za Algeria na Sudan na kudai kuwa hali kama hiyo inawezekana kutokea nchini DRC.

Fayulu amesema amerejea nyumbani kuongeza shinikizo kwa rais Tshisekedi anayemtuhumu kuwa ameiuza nchi na kuwa mtumwa wa chama kilichokuwa madarakani cha rais Joseph Kabila.

Matamshi ya Fayulu yamekuja wakati huu rais Tshisekedi akitafuta uungwaji mkono kutoka kwa wananchi kama sehemu ya kutafuta maridhiano baada ya uchaguzi ulioshuhudia akitangazwa mshindi, huku chama chake kikiwa hakina umiliki wa Bunge la kitaifa wala Seneti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.