rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Comoro Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Maeneo kadhaa ya Comoro yaathirika na kimbunga Kenneth

media
Wacomoro wafungua ukurasa mpya baada ya kimbunga Kenneth kupiga katika maeneo kadhaa, Moroni, Aprili 25, 2019. © Ibrahim YOUSSOUF / AFP

Raia kutoka baadhi ya maeneo nchini Comoro wanaendelea kusubiri msaada siku moja baada ya kimbunga Kenneth kupiga maeneo yao usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii.


Kimbunga Kenneth kimesababisha vifo vya watu wawili, kwa mujibu wa mamlaka na nyumba kadhaa zimeharibika vibaya. Kimbunga hiki pia kimesababisha uharibifu mkubwa mashamba na barabara kadhaa sasa hazipitiki, kwa mujibu wa mashahidi.

Serikali bado ina kazi ngumu ya kukarabati barabara na kutoa msaada kwa watu waliopoteza makaazi yao.

"Hatukuwahi kufikiri kuwa kutatokea kimbunga kama hiki. Tangu mwaka 1959, hatujawahi kushuhudia kimbunga kama hiki kilichotokea hapa Comoro. Nyumba nyingi zimeporomoka kufuatia mafuriko na upepo mkali vilivyosababishwa na kimbunga Kenneth, " amesema mkaazi moja."

Serikali ya Comoro imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia raia wake walioathiriwa na kimbunga Kenneth.