Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Sudan: Jeshi lafikia makubaliano na viongozi wa waandamanaji

Mazungumzo yanaendelea kati ya viongozi wa maandamano na Baraza la Kijeshi nchini Sudani. Mkutano kati ya wawakilishi wa jeshi na viongozi wa waandamanaji ulifanyika Jumatano usiku, saa chache kabla ya maandamano makubwa yaliyoitishwa na upinzani kutarajia kuyakumba baadhi ya maeneo ya Khartoum leo Alhamisi.

Waandamanaji wakimiminika mitaani Khartoum, Sudan, Aprili 24, 2019
Waandamanaji wakimiminika mitaani Khartoum, Sudan, Aprili 24, 2019 © REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano huo jeshi limetangaza kufikia "makubaliano kwa mambo mengi miongoni mwa madai ya waandamanaji".

Hatua hii ni mwanzo wa kuendelea na mazungumzo, chanzo kutoka jeshi kimesema. Hofu ilikuwa kuvunjika kwa mazungumzo kati ya muungano wa kiraia unaowakilisha waandamanaji na jeshi linaloshikilia madaraka nchini Sudani baada ya kumtimuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar Hassan al-Bashir.

Siku ya Jumatano jioni, pande hizi mbili ziliafikiana kuunda kamati ya pamoja ili kutatua tofauti zao.

Hata hivyo mazungumzo yao yatajikita hasa kuhusu jeshi kukabidhi madaraka kwa raia, moja ya madai makuu ya waandamanaji na Umoja wa Afrika ambao, hivi karibuni ulitishia kusitisha ushirikiano wake na Sudan kama jeshi halitofanya hivyo.

Wakati huo huo maafisa watatu ambao ni miongoni mwa viongozi wakuu wa Baraza la Jeshi la Mpito wamejiuzulu baada ya kushtumiwa kuwa na ushirikiano wa karibu na utawala uliopinduliwa. Mafisa hao ni Jenerali Zineladine, mkuu wa kamati ya kisiasa ya Baraza la Kijeshi, na maafisa wengine wawili, ikiwa ni pamoja na mkuu wa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.