rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila Felix Tshisekedi

Imechapishwa • Imehaririwa

Jeanine Mabunda achaguliwa kuwa Spika wa Bunge DRC

media
Jeanine Mabunda Lioko (PPRD - FCC) Kati ya kura 383, amepata kura 375. Anamrithi Aubin Minaku Ndjalandjoko (PPRD) Assemblée Nationale/twitter.com

Wabunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemchagua Jeanine Mabunda kutoka muungano wa FCC kuwa Spika mpya wa Bunge.


Bi. Mabunde alikuwa mgombe pekee baada ya mpinzani wake Henri Thomas Lokondo, kuondolewa na zoezi hilo kususiwa na wabunge wa upinzani wakisema zoezi hilo halikuwa huru na haki.

Spika mpya anatokea muungano wa siasa unaomuunga mkono rais wa zamani Joseph Kabila na anakuwa mwanamke wa kwanza, kuchaguliwa katika nafasi hiyo.

Hata hivyo, Lokondo aliyeondolewa katika uchaguzi huo amesema alikuwa na uhakika wa kushinda.

Wakati huo huo vyama vya upinzani vinavyojumuika kwenye muungao wa CASH wa rais Felix Tshisekedi wamejitoa kwenye kamati kuu ya Bunge wakisema kuwa wamenyimwa nafasi zao walizoahidiwa kwenye Bunge.

Hata hivyo wabunge kutoka vyama hivyo wamesema wataendelea kushiriki vikao vya bunge, kwa kutekeleza majukumu waliopewa na wananchi.