Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-RUSHWA

Serikali mpya DRC kutangazwa hivi karibuni

Baada ya kukabidhiwa madaraka miezi mitatu iliyopita, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo ameahidi kwamba hivi karibuni serikali mpya itatangazwa.

Rais wa DRC Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo amesema serikali mpya itatangazwa hivi karibuni.
Rais wa DRC Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo amesema serikali mpya itatangazwa hivi karibuni. REUTERS/ Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo amelitoa akiwa ziarani Kisangani Jumanne wiki hii.

Hii inakuja siku moja baada ya kukutana kwa mazungumzo na mtangulizi wake Joseph Kabila Kabange kuhusu uteuzi wa waziri mkuu.

Félix Tshisekedi aliwasili Kisangani katika Jimbo la Tshopo Jumanne wiki hii kama sehemu ya ziara yake kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ili kutathmini miradi ya maendeleo nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya rais jijini Kinshasa rais Félix Tshisekedi ameenda Kisangani kuzindua miradi ya maendeleo ikiwemo, ukarabati wa miundo mbinu kama mabarabara pamoja na kuanzishwa upya kwa ujenzi wa madaraja mawili kwenye Miito Lubunga na Wanyarukula,

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, serikali ya jimbo la Tshopo ilisema kuwa rais Tshisekedi amezindua rasmi daraja kubwa la Lubuya lenye urefu wa mita takribani thelathini, kwenye mto Wanyerukula ulioko kilomita 54 kutoka mji wa Kisangani kwenye barabara ya Lubutu.

Daraja hilo linaunganisha mikoa ya Maniema na ule wa Tshiopo, na ni muhimu kwa kurahisisha shughuli za kibiashara.

Inaarifiwa kuwa ujenzi wa daraja hilo umefadhiliwa na serikali kupitia Mfuko wa Kukuza Viwanda (FPI) ikitarajiwa kuwa litaunganisha mikoa ya kivu Kaskazini na Kusini, Maniema na Tshopo miaka 50 baada ya kuporomoka kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.