rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kusini Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Mvua zaua watu zaidi ya 50 Afrika Kusini

media
Mvua zinazonyesha Afrika kusini zimesababisha maafa makubwa na uharibifu katika mikoa miwili ya nchi hiyo, KwaZulu-Natal na Durban. REUTERS/Gavin Welsh

Mafuriko na maporomoko ya udongo yanayosababishwa na mvua zilizonyesha katika siku za hivi karibuni, kusini mashariki mwa Afrika Kusini, zimesababisha watu wengi kupoteza maisha, mamlaka imesema Jumatano wiki hii.


Shughuli za uokoaji zinaendelea kutafuta manusura na miili ya waathirika katika majengo yaliyoanguka katika eneo la pwani la jimbo la KwaZulu-Natal, ambako idadi ya vifo imeongezeka hadi 51, viongozi katika eneo hilo wamesema.

Mvua kubwa zinanyesha katika eneo hilo kwa siku kadhaa. Siku ya Jumatatu viongozi walisitisha ziara yao katika eneo la KwaZulu-Natal kutokana na kuharibika kwa barabara, Lennox Mabaso, msemaji wa serikali ya mkoa amesema.

Watu wengi wameangukiwa na nyumba, huku barabara kadhaa zikiharibika kwa mafuriko, hasa katika mji wa Durban na vitongoji vyake.

Watu watatu pia wamepoteza maisha kufuatia mafuriko katika jimbo jirani la Mashariki mwa Cape, kwa mujibu wa kituo habari cha serikali cha SADC.

Ofisi ya Rais Cyril Ramaphosa imesema rais huyo anatarajia kuzuru mikoa miwili iliyoathirika na mvua hizo zinazoendelea.