Pata taarifa kuu
MISRI-KATIBA-SIASA

Misri: Katiba mpya ya rais Sissi yapitishwa kwa 88% ya kura

Matokeo ya kura ya maoni nchini Misri yameonyesha kuwa Wananchi wa Misri wameunga mkono kufanyika mabadiliko ya katiba yatakayo mruhusu Rais Abdel-Fatah el-Sissi kubakia madarakani hadi mwaka 2030, kwa asili mia 88.5 ya kura zote.

Maafisa wa Tume ya Uchaguzi ya Misri wakitangaza matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Misri katika mkutano na waandishi wa habari, Cairo Aprili 23, 2019.
Maafisa wa Tume ya Uchaguzi ya Misri wakitangaza matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Misri katika mkutano na waandishi wa habari, Cairo Aprili 23, 2019. MOHAMED EL-SHAHED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kama ilivyotarajiwa, "ndiyo" imepita katika kura ya maoni ya Katiba ya Misri, Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi imetangaza.

Rais Abdel Fattah al-Sisi hatimaye atasalia madarakani hadi mwaka 2030, na jeshi litasimamia uheshimishaji wa Katiba.

Watu zaidi ya milioni 26, sawa na 88% ya wapiga kura wameamua na kupiga kura ya "ndiyo" kwa kubadilisha Katiba.

Jambo muhimu zaidi kwa utawala ni ushiriki wa wapiga kura, 44% kwa jumla ya wapiga kura milioni 61.Hatua hii ni muhimu zaidi kwa utawala. Kiwango hiki bora kuliko wakati wa kura ya maoni ya Katiba mnamo mwaka 2014, ambapo kiwango cha ushiriki kilifikia 39% - na mnamo mwaka 2012, kiwango cha ushiriki kilifikia 41%.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa kura hiyo ya maoni iliitishwa wakati wakosoaji wa Al -Sisi wakiandamwa na nguvu za dola.

Serikali ya Misri inaendelea kuwazuia jela maelfu ya watu, wengi wao wakidaiwa ni wafuasi wa itikadi kali ingawa wachambuzi wanaeleza kuwa kuna wanaharakati wa kawaida pia kati ya hao walioko jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.