rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

Algeria Abdelaziz Bouteflika Abdelkader Bensalah

Imechapishwa • Imehaririwa

Vyama vya upinzani vyasusia mazungumzo yaliyoandaliwa na utawala Algeria

media
Wajumbe wa mashirika ya kiraia wakishiriki mkutano uliyoitishwa na rais wa mpito wa Algeria, Abdelkader Bensalah, Algiers, Aprili 22, 2019. © RYAD KRAMDI / AFP

Kiongozi wa muda nchini Algeria Abdelkader Bensalah, ambaye aliteuliwa hivi karibuni kumrithi rais Abdelaziz Bouteflika ameunda kamati maalum ambayo kwa mara ya kwanza, Jumatatu wiki hii iliitisha kikao kitakachojadili juu ya uwezekano wa kuahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa Julai 4 mwaka huu.


Hata hivyo baadhi ya vyama vya kisiasa viliamua kususia mkutano huo, kufuatia kile vyama hivyo vinasema unaenda kinyume na matakwa ya wananchi.

"Wananchi wa Algeria wanataka mabadiliko halisi. Hawakubaliana kwamba utawala uendelee kuongozwa na watu waliokuwa chini ya uongozi wa utawala wa rais Abdelaziz Bouteflika. Sote tunaomba Bensalah kuondolewa kwenye nafasi hiyo, anapaswa kuondoka. Ni vizuri kusikia wito wa wananchi wa Algeria na kisha tutaketi kwenye meza ya mazungumzo, " amesema Abderrazak MAkri kiongozi wa chama cha MSP.

Maandamano yameendelea kushuhudiwa nchini Algeria ambapo wananchi wameomba kuondolewa kwa mfumo wote wa utawala uliokuwa chini ya rais aliyelazimishwa kujiuzulu, Abdelaziz Bouteflika.