Pata taarifa kuu
SUDANI-LIBYA-AU-SIASA-USALAMA

Hali ya Sudan na Libya kujadiliwa katika mkutano Misri

Kunatarajiwa kufanyika mikutano miwili ya dharura nchini Misri Jumanne hii, Aprili 23, kuhusu hali inayoendelea nchini Sudani na Libya. Rais Abdel Fattah al-Sisi ataongoza mikutano yote kama Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ataongoza mikutano miwili jijini Cairo kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ataongoza mikutano miwili jijini Cairo kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa kwanza utahusu hali inayoendelea nchini Sudan ambako maandamano ya raia yanaendelea licha ya Rais Omar el-Bashir kutimuliwa mamlakani na jeshi.

Kiongozi mpya, Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, anaongoza Baraza la Jeshi la Mpito.

Nchi kadhaa za Kiarabu, ikiwa ni pamoja na Misri, zimetonyesha uungwaji wao mkono kwa kiongozi huyo mpya wa Sudani. Hata hivyo, waandamanaji wanaendelea kuomba jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Mkutano wa pili utahusu hali inayoendelea nchini Libya ambako mkuu wa majeshi ya ANL, Marshal Khalifa Haftar, aliagiza majeshi yake kuzindua mashambulizi dhidi ya mji mkuu Tripoli, wiki tatu zilizopita. Mji wa Tripoli uko chini ya udhibiti wa majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Marshal Haftar anaungwa mkono na Misri na Saudi Arabia, wakati serikali ya Tripoli inaungwa mkono na Qatar na Uturuki. Pamoja na watu kuendelea kupoteza maisha, wito wa kusitisha mapigano haujatekelezwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limegawanyika juu ya kupitishwa kwa azimio.

Marais wa Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda, Djibouti, Somalia na Afrika Kusini, pamoja na maafisa wakuu wa Ethiopia, Sudan Kusini na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika wanatarajia kushiriki mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.