Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Tshisekedi na Kabila wakutana kuzungumzia uteuzi wa waziri mkuu

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea kusubiri kwa hamu na gamu uteuzi wa waziri mkuu mpya, miezi kadhaa baada ya Antoine Felix Tshisekedi Tshilombo kuchukuwa mikoba ya Joseph kabila Kabange kwenye uongozi wa nchi.

Joseph Kabila na Felix Tshisekedi katika sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa DRC (Tshisekedi), Kinshasa Januari 24, 2019.
Joseph Kabila na Felix Tshisekedi katika sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa DRC (Tshisekedi), Kinshasa Januari 24, 2019. © REUTERS/ Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao walikutana Jumatatu wiki hii na kuzungumzia kuhusu nafasi ya waziri mkuu ambayo imesalia wazi, miezi minne baada ya uchaguzi wa urais uliompa ushindi Felix Tshisekedi na kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.

Awali Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikuwa hawaelewani kufuatia mvutano wa kisiasa uliokuwa iliikumba DRC na kisha baada ya uchaguzi wa urais wawaili hao waliamua kufanya kazi kwa ushirikiano wakiwa katika muungano mmoja wa kisiasa.

Rais Tshisekedi na Joseph Kabila walikuwa hawajakutana kwa wiki kadhaa kutokana na ziara za kikazi za Tshisekedi. Lakini kwa pande zote mbili, wanahakikisha kuwa rais wa sasa na mtangulizi wake huzungumza mara kwa mara.

Mazungumzo kati ya wawili hao kuhusu uteuzi wa waziri mkuu na uundwaji wa serikali yalidumu saa moja.

Kuhusu swala la waziri mkuu, mazungumzo yanaendelea, karibu miezi minne baada ya Felix Tshisekedi kuapishwa kama Rais wa Jamhuri. Mwanzoni, wawili hao walikuwa wamechagua timu za mazungumzo, lakini mazungumzo yao yaliambulia patupu. Mazungumzo sasa yanafanyika katika ngazi ya juu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.