rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

Mali Siasa Saliou Maiga

Imechapishwa • Imehaririwa

Waziri Mkuu wa Mali Soumeylou Boubeye Maiga ajiuzulu

media
Waziri Mkuu wa Mali Soumeylou Boubèye Maïga MICHELE CATTANI / AFP

Waziri mkuu wa Mali Soumeylou Boubeye Maiga ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, siku moja kabla ya wabunge kuupigia kura muswada wa kutokuwa na imani naye.


Hatua ya kujiuzulu kwa Maiga, imekuja baada ya wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala cha RPM nchini humo kuwasilisha mswada wa kutokuwa imani naye.

Mswada huo unatarajiwa kupigwia kura siku ya Ijumaa, ishara kuwa wabunge wengi wamekosa imani na kiongozi huyo.

Baba Dakono, ambaye ni mtafiti katika kituo cha utafiti jijini Bamako anaona kuwa kuondoka kwa Waziri Mkuu kutamdhohofisha rais Ibrahim Boubakar Keita.

Maandamano ya kumtaka waziri mkuu kujiuzulu yalishuhudiwa siku kumi zilizopita ambapo viongozi wa kidini na wapinzani waliandamana kumtaka awachie ngazi kutokana na kuongezeka kwa visa vya ukosefu wa usalama nchini humo.