Pata taarifa kuu
SOMALI-SIASA

Waziri Mkuu wa Mali akabiliwa na shinikizo la kujiuzulu

Wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala cha RPM nchini Mali, siku ya Jumatano wiki hii, wamewasilisha muswada wa kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu nchini Mali Soumeylou Boubeye Maiga.

Waziri Mkuu wa Mali Soumeylou Boubèye Maïga, Oktoba 2018 Mopti.
Waziri Mkuu wa Mali Soumeylou Boubèye Maïga, Oktoba 2018 Mopti. MICHELE CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Muswada huo umewasilishwa na wabunge zaidi ya 140 wanaokidhi vigezo vya kupiga kura, ambao hatua inayofuata ni kupigiwa kura kwa muswada huo wa kutokuwa na imani na waziri mkuu Ijumaa April 19.

Baba Dakono, ambaye ni mtafiti katika kituo cha Utafiti jijini Bamako nchini Mali anaona kuwa kuondoka kwa waziri mkuu kutamdhohofisha rais Ibrahim Boubakar Keita.

Maandamano ya kumtaka waziri mkuu kujiuzulu yalishuhudiwa siku kumi zilizopita ambapo viongozi wa kidini na wapinzani waliandamana kumtaka Soumaylou Boubaye Maiga ajiuzulu kwa kosa la kushindwa kushughulikia maswala muhimu ikiwemo ya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.