rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Felix Tshisekedi Joseph Kabila

Imechapishwa • Imehaririwa

DRC yaendelea kusalia bila serikali

media
DRC: Felix Tshisekedi na Joseph Kabila katika sherehe ya kuapishwa kwa rais Tshisekedi, Januari 24, 2019 Kinshasa (picha ya kumbukumbu). REUTERS/ Olivia Acland

Majadiliano kuhusu uteuzi wa waziri mkuu mpya nchini DRCongo yaonekana kukwama baada ya rais Felix Thisekedi Tshilombo kukataa kumteuwa mtu ambae amependekezwa na kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila.


Albert Yuma mwenyekiti wa shirika la madini nchini DRCongo (Gecamines), ambae anatuhumiwa na mashirika kadhaa kuhusika katika kupitisha mlango wa nyuma mamilioni ye fedha, jambo ambalo amekuwa akilikanusha, ndiye ambae alipendekezwa na kambi ya rasi wa zamani Joseph Kabila.

Matamshi ya rais Felix Tshisekedi wakati wa ziara yake jijini Washington kwamba anakwenda kuondoa mfumo wa kidikteta wa mtangulizi wake, ilikuja kuchochea mvutano ambao tayari ulikuwa umeanza kuchomoza.

April 6 wajumbe wa kambi zote mbili walikubaliana kukutana nje kidogo na jiji la Kinshasa, jambo ambalo kwa asilimia kubwa wajumbe wa kambi ya Kabila hawakushiriki katika mazungumzo hayo, ambayo yanaongozwa na Nehemie Mwilanya upande wa kambi ya rais wa zamani Joseph kabila.

Hata hivyo mazungumzo hayo yameendelea licha ya baadhi ya wajumbe wa kambi ya rais Kabila kutokuwepo na kutamatika bila kufikia muafaka. Lakini kila upande umekataa kuthibitisha kuwa mazungumzo yamekwama.

Kila upande umeendelea kushikilia msimamo wake. Upande wa FCC wameendelea kulazimisha uteuzi wa Albert Yuma, wakidai ni kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo kwamba FCC ndio wanatakiwa kupendekeza jina la waziri mkuu.

Upande wa kambi ya Tshisekedi ambao wako chini ya shinikizo la wafuasi wao wameendelea kushikilia msimamo wao, huku kada mmoja wa FCC akibashiri kuwa huenda mvutano huo ukachukuwa muda mrefu.