Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-UCHAGUZI

Abdelaziz Bouteflika aomba radhi wananchi wa Algeria

Baraza la Katiba limeidhinisha, Jumatano, Aprili 3 jioni, barua ya kujiuzulu ya Abdelaziz Bouteflika. Na jioni, aliyekuwa rais wa nchi hiyo aliomba radhi kwa wananchi wa Algeria katika barua iliyosomwa kwenye vyombo vya habari nchini Algeria.

Abdelaziz Bouteflika wakati wa kuapishwa kwake tarehe 28 Aprili 2014.
Abdelaziz Bouteflika wakati wa kuapishwa kwake tarehe 28 Aprili 2014. © REUTERS/Louafi Larbi/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake, serikali imetangaza mfululizo wa kwanza wa hatua za uwazi kwa vyombo vya habari, upinzani na vyama vya wafanyakazi.

Shirika la Habari la APS lilichapisha Jumatano jioni barua ya Abdelaziz Bouteflika. "Ninaondoka mamlakani na kuachana moja kwa moja na siasa bila masikito yoyote wala hofu yoyote kwa hatima ya nchi yetu," amesema rais mstaafu katika barua yake, na kuwataka wananchi wa Algeria "kudumisha umoja wao".

Pia ameomba "msamaha kwa wananchi wenzake, ambao, bila kukusudia, sikuwajibika kwao au walijikuta walifanyiwa unyonge nilipokuwa mamlakani."

Baada ya karibu miaka miwili madarakani, Abdelaziz Bouteflika pia amesema anajiona mwenye hurafa kwa mchango wake na amekaribisha maendeleo ambayo Algeria imefikia sasa.

Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi.

Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma.

Kuondoka madarakani kwa kiongozi huyo pia kumekuja baada ya kiongozi wa maandamano kukataa ahadi iliyotolewa na Rais Bouteflika wiki hii kwamba atajiuzulu madarakani ifikapo Aprili 28.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.