rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Algeria Abdelaziz Bouteflika

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa Algeria Bouteflika aachia ngazi

media
Abdelaziz Bouteflika mnamo mwaka 2009 mbele ya wafuasi wake huko Blida. © Fayez Nureldine / AFP

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amejiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia shinikizo la maandamano yaliyoanza tangu alipotangaza kuwania muhula wa tano katika uchaguzi ujao ambao umesogezwa mbele kwa tarehe isiyojulikana.


Hatua hii imekuja saa chache baada ya kuahidi kuwa angefanya hivyo kabla ya muda wake kukamilika tarehe 28 mwezi huu.

Amelazimika kuchukua hatua hii kutokana na shinikizo za wananchi ambao tangumwezi Februati wamekuwa wkaiandamana wkaimtaka Biuteflika mwenye umri wa miaka 82 kuachia madaraka baada ya kutangaza kuwa angewania tena uongozi wa taifa hilo kwa muhula wa tano.

Raia wa Algeria wamekuwa wakisherehekea hatua hii na kusema ni hatua ya kwanza ya ushindi na wataendelea na maandamano kuhakikisha jopo zima la Bouteflika linaondoka.

Kuondoka madarakani kwa kiongozi huyo pia kumekuja baada ya kiongozi wa maandamano kukataa ahadi iliyotolewa na rais Bouteflika wiki hii kwamba atajiuzulu madarakani kabla ya Aprili 28.

Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma.

Rais Abdelaziz Bouteflika, ameweza kutoa taarifa hizo rasmi kwa mujibu wa katiba inayoruhusu rais kusitisha muda wake wa kutawala.

Jeshi nchini humo limechangia pakubwa kuhakikisha Rais Bouteflika anaondoka haraka iwezekanavyo baada ya kuahidi kuwa atajiuzulu kabla ya April 28.