rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Maandamano nchini Iraq: Takwimu rasmi za watu waliouawa ni 157, pamoja na 111 Baghdad
  • Machafuko Chile: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 15 baada ya watu watatu kuuawa (serikali)
  • Rais wa Chile PiƱera ajaribu kutuliza hasira za waandamanaji baada ya maandamano mapya

Malawi Afrika Kusini

Imechapishwa • Imehaririwa

Raia wa Malawi waishio Durban waomba kurudishwa nyumbani

media
Maelfu ya Waafrika Kusini wakiandamana Johannesburg kueleza kupinga ubaguzi dhidi ya wageni, Aprili 23, 2015. REUTERS/Mike Hutchings

Baadhi ya raia wa Malawi wanaoishi mjini Durban nchini Afrika Kusini, wameomba kurudishwa nyumbani. Hatua hiyo inakuja baada ya kushambuliwa na raia wa Afrika Kusini.


Uvamizi wa raia hao wa kigeni ulisababisha wananchi wa Malawi wapatao 300 kuyakimbia makaazi yao.

Makaazi yao yalivamiwa na biashara zao kuharibiwa na wenyeji, suala ambalo limeikasirisha serikali ya Afrika Kusini na kuwataka maafisa wa usalama kuwakamata na kuwachukulia hatua waliohusika.

Wimbi la raia wa Afrika Kusini kuwavamia raia wa kigeni kutoka mataifa mengine ya Afrika, limeendelea kuzua wasiwasi nchini humo.

Mapema Jumatatu watu watatu walifariki kufuatia maandamano yanayolenga maduka, mengi ambayo yanamilikiwa na wageni.

Takriban watu 50 walitafuta hifadhi katika kituo kimoja cha polisi wakati kundi moja la vijana wa Afrika wasio na kazi walipowashinikiza kutoka katika majumba yao usiku.

Siku ya Jumatatu wiki hii waziri wa mamabo ya kigeni nchini Afrika Kusini alikutana na mabalozi na kusema kuwa ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na raia wengi wa Afrika katika jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia hususan katika mkesha wa siku ya mwezi wa uhuru ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 25 tangu uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo.