Pata taarifa kuu
DRC-VYOMBO VYA HABARI-UCHUMI

Vyombo vya habari DRC vyakumbwa na sintofahamu

Kufuatia hali ya uchumi nchini DRC, vituo vya televisheni Digital-Congo na Tele 50 vimeshindwa kulipa mishahara wafanyakazi wao kwa miezi kadhaa sasa.

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa (picha ya kumbukumbu).
Mji mkuu wa DRC, Kinshasa (picha ya kumbukumbu). © CC 2.0/MONUSCO/Myriam Asmani
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa zamani na washirika wa karibu wa Joseph Kabila, wameanza kutafuta usuluhu. Vituo hivyo viwili vilianza kukumbwa na hali hiyo baada ya kujiuzulu kwa Moïse Katumbi kama gavana wa mkaa na mkuu wa chama cha PPRD katika mkoa wa Katanga. Alikuwa mojawapo wa wachangiaji wakubwa katika vituo hivi viwili ambavyo vilikuwa karibu na utawala wa zamani wa Joseph Kabila, mbali na kituo cha serikali cha RTNC.

Madai ya wafanyakazi wa Digital Congo na Tele 50 yaliongezeka baada ya mabadiliko katika uongozi wa nchi hiyo. Baada ya kukusanya miezi kadhaa ya madeni ya mishahara, wafanyakazi wa vituo hivi viwili, pia, walianza kujiunga na wenzao katika migomo ya kila mara, kama katika makampuni mengine mengi nchini DRC.

"Tutalipa awamu ya kwanza ya malimbikizo ya mishahara kwa wafanyaazi wa Digital kabla ya siku ya Jumamosi, malipo ya awamu nyingine yatafanyika kabla ya mwezi Juni mwaka huu," amesema Theodore Mugalu. Mkuu wa makaazi ya aliyekuwa rais wa DRC Joseph kabila, ametangaza pia kwamba watapitia upya uongozi wa Digital Congo. Kwa upande wa Tele 50, hali bado ni tete.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.