Pata taarifa kuu

Rais wa DRC Felix Tshisekedi azuru Rwanda

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi, anazuru Rwanda na leo ametembelea eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbari jijini Kigali.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Luanda, Angola, Februari 5, 2019.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Luanda, Angola, Februari 5, 2019. Stringer/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii imekuja, wiki mbili kuelekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kutokea kwa mauaji hayo mabaya yaliyotokea mwaka 1994 na kusababisha zaidi ya watu 800,000 kupoteza maisha. Hii ni ziara ya kwanza kwa rais Tshisekedi baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa DRC. Rwanda na DRC ni mataifa jirani ambayo yanashirikiana kibiashara lakini suala la usalama mipakani linasalia changamoto.

Kwa upande mwengine rais wa Rwanda Paul Kagame, ameishtumu Uganda kwa kuiwekea vikwazo vya kufanya biashara, suala ambalo amesema linakwenda kinyume na makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ameishtumu Uganda, kwa kuzuia bidhaa kutoka Rwanda kwa sababu ambazo amezieleza kuwa hazina uzito na hivyo kuharibu biashara.

Kagame amelalamikia mizigo ya nchi yake inayotokea Bandari ya Mombasa kuzuiwa kwa zaidi ya miezi mitano, sawa na maziwa yaliyokua yanakwenda Kenya kuzuiwa kwa siku kadhaa na kuharibika, suala ambalo amesema ni siasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.