Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga Idai: Shughuli ya uokoaji yaendelea Msumbiji

Waokoaji nchini Msumbiji wanasema wamewafikia maelfu ya raia waliokwama kwa wiki moja tangu kimbunga cha Idai kilipopiga nchini humo na mataifa ya Malawi na Zimbabwe.

Familia moja iliyokimbilia kwenye paa ya nyumba yao katika Wilaya ya Buzi, Msumbiji, Machi 21, 2019.
Familia moja iliyokimbilia kwenye paa ya nyumba yao katika Wilaya ya Buzi, Msumbiji, Machi 21, 2019. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja wakati serikali ya Msumbiji ikitangaza kufunguliwa kwa miundombinu ikiwemo barabara katika maeneo yaliyoathirika.

Waziri wa Mazingira na Ardhi wa Msumbiji Celso Correira ameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa serikali inaendelea kutoa chakula na mavazi kwa zaidi ya watu laki moja waliookolewa.

Kimbunga idai kilichopiga Mji wa beira na kusambaa katika nchi za Malawi na Zimbabwe na kuuwa watu zaidi ya mia sita.

Afisa kutoka ofisi inayoratibu misaada ya kibinadamu ya umoja wa mataifa, Sebastian Rhodes Stampa amesema visa vya maradhi ya kuhara na idara yake inafuatilia kwa karibu uwezekano wa kuibuka kwa visa vya maradhi ya kipindupindu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.