Pata taarifa kuu
DRC-YUMBI-MAUAJI-USALAMA

Mauaji Yumbi: Serikali ya DRC yahusisha maafisa wake

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekubali kwa mara ya kwanza kuwa, viongozi wa serikali katika eneo la Yumbi Magharib mwa nchi hiyo, walichangia kuuawa kwa mamia ya watu mwezi Desemba mwaka uliopita.

Moja ya nyumba zilizochomwa moto wakati wa machafuko yaliyokikumba kijiji cha Yumbi Desemba, 2018.
Moja ya nyumba zilizochomwa moto wakati wa machafuko yaliyokikumba kijiji cha Yumbi Desemba, 2018. RFI/Patient LIGODI
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yalitokea katika vijiji vitatu kwa siku mbili, watu 535 walikuwa wameuawa kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mashirika ya Kimataifa.

Waziri wa masuala ya haki za binadamu nchini DRC Marie-Ange Mushobekwa amesema, serkikali ya Kinshasa inatambua kuwa maafisa wake walihusika.

Umoja wa Mataifa ulibainisha katika ripoti yake ya Machi 12 kwamba machafuko yaliyotokea katika eneo la Yumbi ni sawa na uhalifu dhidi ya binadamu.

Yumbi ni wilaya ya mkoa wa Mai-Ndombe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo katikati mwa mwezi Desemba, kabla tu ya kufanyika Uchaguzi Mkuu kulitokea mashambulizi mabaya yaliyosababisha vifo vya watu 535 upande wa jamii ya Banunu.

Machafuko ya kikabila yalitokea pia wakati jamii moja ilipotaka kuzika mmoja wa viongozi wao wa kitamaduni katika ardhi ya jamii nyingine.

Aidha uchunguzi huo ulionesha pia vurugu zinaweza kuibuka tena wakati wowote.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walifahamisha kwamba ghasia zilizotokea kati ya Desemba 16 na 18 zilikuwa zimepangwa.

Jamii ya kabila la Batende walivamia na kushambulia vijiji vya wawatu kutoka jamii ya Banunu, na watu wachache tu ndio waliofanikiwa kutoroka.

Taarifa hiyo, iliongeza pia kwamba mamlaka katika eneo la Yumbi, kwenye jimbo la Mai-Ndombe, magharibi mwa nchi, zilishindwa kuwajibika kwa kuwalinda raia.

Timu hiyo ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliweza kuvifikia katika vijiji vitatu kati ya vinne, wakati mashambulizi yalipopamba moto.

Miili ya watu inaaminika pia ilitupwa katika mto Congo.

Ripoti hiyo ilisema kuwa takriban watu 500 waliuawa ikiwemo baadhi ya familia zilizochomwa moto ndani ya nyumba zao na mtoto wa miaka miwili kutupwa ndani ya tanki la maji machafu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.