Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Wananchi wa Algeria waendelea kuandamana

Wanafunzi, mahakimu na waandishi wa habari nchini Algeria wamekusanyika Jumapili, Machi 17 kote nchini baada ya majuma manne ya maandamano.

Raia wa Algeria waishio Ufaransa wanaunga mkono ndugu zao wanaoandamana nchini Algeria wakati wa mkutano wao Paris Machi 17.
Raia wa Algeria waishio Ufaransa wanaunga mkono ndugu zao wanaoandamana nchini Algeria wakati wa mkutano wao Paris Machi 17. © Geoffroy VAN DER HASSELT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Upinzani unamtaka rais Abdelaziz Bouteflika kuondoka madarakani, jambo ambalo limeonekana kutosikilizwa na viongozi ambao tayari wamewasilisha mapendekezo ya kipindi cha mpito.

Hayo yanajiri wakati huu upinzani na raia wa Ufaransa wenye asili ya Algeria wakiandamana na kuahidi kutochoka kuendelea na maandamano kumtaka rais Boutekflika kusikiliza wito wa wananchi.

Baadhi ya waandamanaji waliojitokeza wameeleza mpango wao wa kwenda Algeria kuonyesha ushirikiano zaidi katika maandamano ya siku ya Ijumaa ijayo.

Maandamano ya kuunga mkono wananchi wa Algeria yameshuhudiwa katika miji kadhaa nchini Ufaransa, ikiwemo jiji la Paris, Marseille, Toulouse na Bordeaux.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.