rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Zimbabwe Majanga ya Asili Msumbiji Malawi Emmerson Mnangagwa

Imechapishwa • Imehaririwa

Kimbunga Idai chaua watu 65 Zimbabwe

media
Picha hii iliyopigwa tarehe 15 Machi, 2019 inaonyesha gari wakati mvua ikishesha, mvua ambayo inaaminika kuwa ndio mwanzo wa kimbunga Ida kutoka Msumbiji. AFP

Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Zimbabwe katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Idai kilichokumba maeneo mbalimbali nchini humo kikiwa na mwendo kasi wa kilomita 177 kwa saa.


Watu 65 wamekufa Mashariki mwa Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga hicho.

Rais Emmerson Mnangagwa amelazimika kusitisha ziara yake mashariki ya kati ili kurejea nchini mwake kutokana na janga hili.

Jitihada za uokoaji zinaendelea huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani walioko,hali inahofiwa kwamba huenda inaweza ongeza idadi ya waliopoteza maisha.

Kimbunga Idai kimesababisha uharibifu wa miundo mbinu katika jimbo la Manicaland karibu na mpaka wa Zimbabwe na Msumbiji.

Mashahidi wanasema kasi ya kimbunga hicho inapungua, japo kuwa tayari kimesababisha madhara makubwa huku takribani watu 200 wakiwa hawajulikani walipo.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kimbunga Idai kimesababisha vifo vya watu 120 nchini Msumbiji na Malawi.