Pata taarifa kuu
MALI-JESHI-MAUAJI-KAMBI

Watu wenye silaha wavamia kambi ya jeshi nchini Mali na kusababisha mauaji

Watu wenye silaha wamevamia kambi ya jeshi ya Dioura  nchini Mali na kuwauawa wanajeshi wanane na kuharibu magari matano katika jimbo la Mopti siku ya Jumapili.

Gari la kubeba wagonjwa la Umoja wa Mataifa nchini Mali
Gari la kubeba wagonjwa la Umoja wa Mataifa nchini Mali AP Photo/Baba Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yamethibitishwa na Meya wa mji wa Mopti Youssouf Coulibaly ambaye alitembelea kambi hiyo na kusema kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Kanali wa jeshi la Mali Diarran Kone, naye pia yamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, lakini hakutoa taarifa zaidi.

Maeneo ya Kaskazini na Katikati ya Mali, yameendelea kushuhudia mashambulizi ya kijihadi hasa dhidi ya wanajeshi tangu mwaka 2012.

Changamoto za kiusalama, zilianza kushuhudiwa baada ya waasi wa Tuareg kuanza kudhibiti maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo wakipinga serikali ya Bamako.

Serikali ya Ufaransa imetuma zaidi ya wanajeshi elfu nne, kwenda kukabiliana na makundi ya kijihadi, katika eneo la Sahel, ikiwemo nchi za Burkina Faso, Mauritania, Chad na Niger.

Licha ya kuwepo kwa wanajeshi hao, serikali ya Mali imeshuhudia mashambulizi 237 mwaka 2018 pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.