Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Serikali ya Algeria: Tuko tayari kuzungumza na upinzani

Serikali ya Algeria imesema iko tayari kufanya mazungumzo na upinzani, Naibu Waziri Mkuu Ramtane Lamamra ametangaza Jumatano wiki hii.

Naibu Waziri Mkuu Ramtane Lamamra.
Naibu Waziri Mkuu Ramtane Lamamra. AFP/Farouk Batiche
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Ahmed Gaïd Salah, Mkuu majeshi ya Algeria na Naibu Waziri wa Ulinzi, kwa upande wake amebainisha leo Jumatano kwenye kituo cha televisheni Ennahar kwamba Jeshi la Taifa (ANP) litalinda "katika hali zote "usalama wa nchi.

Baada ya majuma kadhaa ya maandamano, rais Abdelaziz Bouteflika, mwenye umri wa miaka 82, ambaye anakabiliwa na maradhi ya kiharusi tangu mwaka 2013, alitangaza Jumatatu usiku kwamba ahatowania tena muhula wa tano katika uchaguzi wa urais ambao umesogezwa mbele kwa tarehe isiyojulikana. Uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika tarehe 18 Aprili mwaka huu.

Uamuzi huo ulikaribishwa Jumatatu jioni na wananchi wa Algeria pamoja na upinzai.

Lakini maelfu ya waandamanaji wameendelea kuandamana katika miji mbalimbaliwakiomba mageuzi ya haraka, wakihofia kuwa huenda waliokaribu na Bouteflika wakishikilia uongozi wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.