Pata taarifa kuu
UFARANSA-DJIBOUTI-USHIRIKIANO

Rais wa Ufaransa aendelea na ziara yake katika pembe ya Afrika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili nchini Djibouti tangu Jumatatu jioni. Hii ni ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa nchini Djibouti baada ya Nicolas Sarkozy mnamo mwaka 2010.

Moja ya mitaa ya Djibouti (picha ya kumbukumbu).
Moja ya mitaa ya Djibouti (picha ya kumbukumbu). © Wikimedia Creative Commons/CC BY 3.0
Matangazo ya kibiashara

Nchini Djibouti rais Macron anatarajia kutuma ujumbe kwa mshirika wa kihistoria wa Ufaransa katika Pembe ya Afrika wakati kanda hiyo inakabiliwa na hali tete.

"Uhusiano kati ya Ufaransa N Djibouti umeimarika katika miezi ya hivi karibuni. Hivyo ndivyo anavyosema mtaalamu wa kanda hiyo, huku akibaini kwamba kwa leo uhusiano umeimarika zaidi kuliko siku za nyuma. yote hayo ni kutokana na juhudi za Emmanuel Macron, ameomngeza mtaalamu huyo.

François Hollande alisubiri wiki za mwisho za muhula wake ili kumpokea mwenzake wa Djibouti Ismaël Omar Guelleh jijini Paris, wakati wa mkutano wa siri uliofanyika bila taarifa rasmi. Rais wa Djibouti alikuwa tayari amelalamika mnamo mwaka 2015 kuona nchi yake imetengwa na Ufaransa.

Baada ya mazungumzo na mwenzake wa Djibouti Ismaïl Omar Guelleh, ambaye yuko madarakani tangu mwaka 1999, rais wa Ufaransa atazuru kambi ya jeshi la Ufaransa yenye askari 1,500, kikosi kikubwa cha askari wa Ufaransa barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.