Pata taarifa kuu
DRC-ICC-BEMBA-HAKI

Jean-Pierre Bemba aomba alipwe fidia na ICC kwa kufungwa bila hatia

Aliyekuwa Makamu wa rais nchini DRC, Jean-Pierre Bemba, na ambaye alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ameachiwa huru, na amedai mahakama hiyo imlipe zaidi ya euro milioni 68 kama fidia, mwanasheria wake amesema.

Makamu wa zamani wa rais DRC Jean-Pierre Bemba.
Makamu wa zamani wa rais DRC Jean-Pierre Bemba. REUTERS/JERRY LAMPEN
Matangazo ya kibiashara

Upande wa utetezi umesema Jean-Pierre Bemba ameomba mahakama hiyo ya Kimataifa ya ICC imlipe kiasi cha euro milioni 68 kama fidia, kufwatia uharibifu wa mali zake.

Aidha anadai mahakama hiyo kufidia kutelekezwa kwa ndege zake saba na uharibifu wa majengo yake matatu ya kifahari nchini ureno.

Mwanasiasa huyo maarufu nchini DRC anasema ndege zake zilipigwa marufuku tangu kukamatwa kwake na kuzuiliwa na mahakama huko Hague, unchini Uholanzi.

Bemba aliachiwa baada ya kushinda rufaa aliyokata kwenye mahakama hiyo kupinga adhabu ya kifungo cha miaka 18 jela baada ya kukamatwa nchini Ubelgiji mwaka 2016.

Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi mwaka 2016 kwa makosa ya uhalifu, yaliyotekelezwa na wapiganaji wake katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.

Mwezi Juni mwaka jana majaji wa ICC waliagiza Bemba aachiwe huru kwa masharti baada ya kufutiwa mashtaka ya makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.