rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Ulaya Amerika

Imechapishwa • Imehaririwa

Ulimwengu waadhimisha siku ya wanawake duniani

media
Siku ya wanawake duniani inaadhimishwa wakati wanawake wengi wanakabiliwa na hali duni ya maisha huku wengine wakilazimika kukimbilia katika makambi ya wakimbizi kutoka na na migogoo ya kisiasa. ©HCR/Corentin Fohlen

Leo Ijumaa Machi 8 ni siku ya Kimataifa ya Wanawake, siku ambayo dunia inathamini mchango wa wanawake katika jamii na kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwapa wanawake na wasichana nafasi ya kuja na sera ya huduma mbalimbali zitakazosaidia kubadilisha maisha ya watu.


Hata hivyo, wanawake barani Afrika wameendelea kulalamika ubaguzi na uonevu katika masuala mengi hasa uongozi.

Kila mwaka wa tarehe 8 mwezi Machi,wanawake hukumbukwa kwa kuwa huwa ni siku iliyotengwa kwa ajili yao.

Kwa mujibu wa mwanamke mmoja aliyehojiwa na idhaa ya Kiswahili ya RFI mjini Bujumbura nchini Burundi, wanawake wanatambulika kuwa watu muhimu zaidi katika jamii.

“Jamii inayompuuza mwanamke katika shughuli za kimaendeleo huwa ni jamii isiyo na ustaarabu. Mwanamke akihusishwa katika shughuli za maendeleo ya jamii husaidia kuinua jamii hiyo na kuonekana ustaarabu katika jamii husika, “ amesema mwanamke huyo ambaye hakutaja jina lake.

“Mwanamke akiwekwa mstari wa mbele katika jamii basi husaidia katika kuendelea mbele kwa jamii hiyo. Wanawake husaidia katika uzalishaji wa jamii. Haki za wanawake hazifai kuwekwa kando na tathmini ya haki za binadamu” ameongeza.