Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Miji kadhaa kukumbwa na maandamano makubwa Algeria

Raia nchini Algeia wanatarajia leo Ijumaa kumiminika mitaani katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kupinga muhula wa tano wa rais Abdelaziz Bouteflika, ambaye afya yake inaendelea kuzorota.

Abdelaziz Bouteflika akiwa ameongozana, upande wa kushoto mbele, na ndugu yake mdogo na mshauri wake mwandamizi, Saïd, wakati wa uchaguzi wa Aprili 17.
Abdelaziz Bouteflika akiwa ameongozana, upande wa kushoto mbele, na ndugu yake mdogo na mshauri wake mwandamizi, Saïd, wakati wa uchaguzi wa Aprili 17. AFP PHOTO / FAROUK BATICHE
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo rais Abdelaziz Bouteflika ametoa wito hapo Alhamisi wiki hii akitahadharisha waahdamanaji kuhusu uwezekano wa kutokea kwa machafuko.

Kupitia ujumbe uliochapishwa na kituo cha habari cha kitaifa nchini Algeria cha APS, rais Bouteflika kwanza amewapongeza waandamanaji kwa kuandamana kwa amani kudhihirisha dukuduku lao, na kutoa wito wa kuwa waangalifu kuhusu watu ambao wanaweza kujipenyeza na kuanzisha machafuko.

Ally Benfils ni miongoni mwa wapinzani waliojiendoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi amepongeza waandamanaji na kuelezea kuhusu hatari iliopo inayosababishwa na muhula wa 5 wa Abdelaziz Bouteflika.

Abdelaziz Bouteflika alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1999, afya yake ilianza kutetereka tangu mwaka 2013 baada ya kupata kiharusi na hadi anawasilisha fomu ya kuwania uchaguzi yupo nchini Usuisi ambako anapatiwa matibabu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.