Pata taarifa kuu
CAR-SIASA-USALAMA

Umoja wa Afrika watoa wito wa utulivu kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Umoja wa Afrika ambao ulihusika katika kusimamia makubaliano ya amani ya Kharthoum baina ya makundi ya waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati na serikali ya nchi hiyo, umetowa wito wa utulivu.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa "utulivu na kujizuia" nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa "utulivu na kujizuia" nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Flickr/CC/Chatham House/©Suzanne Plunkett 2017
Matangazo ya kibiashara

Wito huo unakuja wakati huu baadhi ya mawaziri wa serikali mpya ilioundwa mwishoni mwa juma kutangaza kujiuzulu kutokana na makundi kadhaa ya waasi kutangaza kutorodhia uundwaji wa serikali hiyo ambayo ilitakiwa kuwa ya kitaifa.

Kati ya makundi 14 yaliosaini makubaliano, sita pekee ndio waliopewa wizara katika serikali ilioundwa Jumapili iliopita. Tayari mawaziri 7 wametangaza kujiuzulu.

Umoja wa Afrika ambao ulisimamia mazungumzo hayo ya Kharthoum umetowa wito wa Utulivu na kuwataka wadau mbalimbali kujizuia na lolote ambalo linaweza kuwa sababu ya kukwama kwa mazungumzo hayo.

Jumatano wiki hii, makundi sita kati ya 14 yaliosaini makubaliano hayo ya Khartoum yalitoa muda wa saa 72 kwa rais na waziri wake mkuu kurejelea upya uundwaji wa serikali hiyo ambayo wanasema haikuzingatia makubaliano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.