Pata taarifa kuu
DRC-CENCO-UTAWALA BORA

CENCO yatoa wito kwa viongozi wapya DRC kurejesha utawala wa kisheria

Baada ya kikao chake cha kawaida cha kamati ya kudumu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Congo (Cenco), baraza hilo limesema limekubaliana na matokeo ya urais, lakini hata hivo limesisitiza ukweli umekataliwa.

Donatien Nshole, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki  DRC (picha ya kumbukumbu).
Donatien Nshole, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC (picha ya kumbukumbu). © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Maaskofu wametoa wito kwa viongozi wapya nchini DRCongo kufanyakazi kwa bidii kurejesha utawala wa kisheria.

Cenco imeendelea kusisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais kama ilivyochapishwa na Tume huru ya taifa ya Uchaguzi (CENI), haifani na takwimu zilizokusanywa na ujumbe wake wa uchunguzi.

Baraza hilo la maaskofu limetangaza kwamba litaendelea na uchunguzi wake wa uchaguzi na mpango wa elimu ya kiraia kama anavyoeleza hapa Dontien Nshole Katibu mkuu wa baraza la maaskofu Cenco.

Hata hivyo upande wa utawala mpya, umesema muda huu sio wa mjadala kuhusu uchaguzi, bali ni muda wa kufanya kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.