Pata taarifa kuu
CAR-SIASA-USALAMA

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yashushiwa lawama

Moja kati ya makundi ya waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati yaliotia saini kwenye makubaliano ya amani kati ya seriali ya Bangui na makundi 14 ya waasi limeituhumu serikali kutoheshimu jukumu lake kwa kuunda serikali bila kuzingatia makubaliano.

MJi mkuu wa JAmhuri ya Afrika ya Kati, Bangui
MJi mkuu wa JAmhuri ya Afrika ya Kati, Bangui REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Chama cha front populaire pour la rennaissence de la centreafrique (FPRC) kimesema katika taarifa yake kwamba viongozi wa serikali wameshindwa kutekeleza makubaliano kwa kuunda serikali mpya, badala yake wamerejesha serikali iliokuwepo.

Mapema Jumapili serikali mpya iliundwa kulingana na makubaliano ya amani ambayo yaliagiza uundwaji wa serikali ya Umoja wa kitaifa, lakini hata hivyo hakuna kilichobadilika washiriki ni walewale.

Kwa mujibu wa Noureddine Adam mwenyekiti wa chama cha FPRC, rais wa Jamauhuri ya Afrika ya Kati amezika matarajio ya wananchi wa taifa hilo ambao walitarajia kuona mabadiliko kwenye nyadhifa mbalimbali.

Kundi hilo limetangaza kuwa halitashiriki kwenye serikali hiyo, licha ya kutoweka wazi kwamba limejitoa kwenye kamati inayofuatilia utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya huko Kharthoum.

Makundi ya waasi ambayo yaliomba kupewa nafasi ya waziri mkuu, jambo ambalo lilitekelezwa, lakini kwenye wizara nyingine muhimu za serikali iliotengazwa kupitia radio ya taifa yamejikuta yametengwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.