rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Siasa Felix Tshisekedi

Imechapishwa • Imehaririwa

Maandamano mjini Goma baada ya watu sita kuuawa

media
Maandamano ya Lucha hivi karibuni, mjini Goma Alain WANDIMOYI / AFP

Watu wenye silaha wameuawa watu sita Mashariki mwa DRC, usiku wa kuamkia Jumapili, mauaji ambayo yamesababisha maandamano ya raia mjini Goma, wakilaani mauaji hayo.

 


Ripoti zinasema kuwa, mauaji hayo yalitokea katika eneo la Ndosho mtaa wa mji wa Goma.

Meya wa mji huo Timothee Muissa Kiense amethibitisha kuuawa kwa watu hao lakini hakuweza kubainisha ni akina nani waliohusika.

"Watu sita walipoteza maisha, baada ya kupigwa risasi na watu tusiowajua," amesema.

"Watu wa mji huu wana hasira sana, kutokana na mauaji haya ambayo hutokea kila wakati," alisisitiza.

Maandamano ya raia yameishumu serikali ya Kivu Kaskazini na Kinshasa kwa kutofanya vya kutosha kupambana ukosefu wa usalama, Mashariki mwa nchi hiyo.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, watu 25 wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha mjini Goma pekee na wengi wanaamini kuwa rais mpya Felix Tshisekedi atasaidia ili utovu wa usalama umalizike.