rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Somalia Al Shabab

Imechapishwa • Imehaririwa

Somalia yaapa kulimaliza kundi la Al Shabab

media
Shambulizi la bomu mjini Mogadishu REUTERS/Feisal Omar

Serikali ya Somalia inasema watu 20 walipoteza maisha siku ya Ijumaa mjini Mogadishu, baada ya kundi la kigaidi la Al Shabab kutekeleza shambulizi ndani ya mkahawa maarufu.


Idadi hiyo imetolewa na serikali ya Mogadishu ambayo imesema, itawasaka magaidi hao na kulipiza kisasi baada ya shambulizi hilo.

Maafisa wa usalama nchini humo kwa saa kadhaa, walipambana na magaidi hao waliokuwa wamewateka baadhi ya watu ndani ya mkahawa huo.

Waziri Mkuu Hassan Ali Khaire amesema kuwa, serikali yake haitachoka kupambana na Al Shabab, kwa gharama yoyote ile.

Mbali na kusababisha maafa na majeraha, mali kama magari ya watu yaliharibiwa katika shambulizi hili la hivi punde nchini humo.

Kundi la Al Shabab limeendelea kuisumbua seriklai ya Somalia, kwa miaka zaidi ya 10 sasa, ikataka kuchukua uongozi wa nchi hiyo.