Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-SIASA

Sudan: Utawala wajaribu kuhakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa

Mapema wiki hii Umoja wa Mataifa, Uingereza, Canada na Norway wamelaani vikali "kurejea kwa utawala" wa kijeshi nchini Sudan baada ya mfululizo wa hatua zilizochukuliwa na rais wa nchi hiyo Omar al-Bashir dhidi ya maandamano yanayomtaka ajiuzulu.

Jenerali Mohammed Ahmed Ibnouf, Makamu wa rais wa Sudan, Oktoba 22, 2018 Khartoum.
Jenerali Mohammed Ahmed Ibnouf, Makamu wa rais wa Sudan, Oktoba 22, 2018 Khartoum. © ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari, Makamu wa rais mpya wa Sudan Jenerali Awad Ibnouf amesema kuwa "hali ya dharura iliyotangazwa na rais Omar al-Bashir hailengi waandamanaji."

Jenerali Ibnouf amebaini kwamba hali ya dharura haiishii kwenye suala la usalama, lakini pia inahusu hali ya kiuchumi ambayo serikali mpya inapaswa kukabiliana ili Sudan iwe na utulivu.

Lakini maneno ya Makamu wa rais wa Sudan yanaonekana kuwa hayawajengi imani wananchi wa Sudan ambao hawana ten aimani na utawala wa sasa.

Raia wameamua kuendelea na maandamano ambayo sasa wameyaita "maandamano ya changamoto" dhidi ya hali ya dharura ambayo inapiga marufuku mkusanyiko wowote.

Wakati Alhamisi hii Februari 28 inasubiriwa kuwa ni siku ya maandamano makubwa nchini Sudan, waandamanaji wametolewa wito kuandamana hadi kwenye ikulu ya rais.

Siku ya Jumatano waandamanaji walipinga hali ya dharura katika miji ya Khartoum na Bahri kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo.

Bunge la Sudan litatahmini hali ya dharura iliyotangazwa na rais Omar al-Bashir siku ya Ijumaa, Machi 6, kwa mujibu wa shirika la habari la Suna. Kulingana na Katiba ya Sudan, Bunge linakubali au kukataa hali ya dharura ndani ya siku 15 baada ya kutangazwa kwake. Uamuzi huu ulizua utata mkubwa nchini na nje ya mipaka ya Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.