Pata taarifa kuu
SENEGAL-SIASA-UCHAGUZI

Tume ya Uchaguzi Senegal yawataka wananchi kuwa watulivu

Kambi ya kampeni ya rais wa Senegal Mack Sall imeendelea kusherehekea kile wanachodai ni ushindi mkubwa wa mgombea wao alioupata katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma, wakati huu upinzani ukikosoa hatua hiyo wakitabiri uchaguzi huo kwenda kwenye duru ya pili.

LZoezi la kuhesabu kura linaendelea Senegal, Februari 24, 2019.
LZoezi la kuhesabu kura linaendelea Senegal, Februari 24, 2019. RFI/Guillaume Thibault
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri saa chache tu baada ya waziri mkuu Mahammed Boun Abdallah Dionne kuibua sintofahamu zaidi baada ya kutangaza kuwa Sall ameibuka mshindi saa chache tu baada ya kufungwa kwa zoezi la upigaji kura.

Hata hivyo waziri mkuu Dionne anasisitiza kuwa matokeo waliyonayo yanathibitisha kauli yake.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (CENA), amefutlia mbali ushindi huo na kusema kuwa matokeo rasmi ya awali yanatarajiwa kutangazwa na mamlaka husika (CENA) na matokeo kabili yatatangazwa na Mahakama ya Katiba.

Kwa upande wake mkuregenzi wa kampeni za mgombea Osumani Sonko, Boubakary Camara anasema kinachofanywa na Serikali ni kujaribu kutengeneza mzozo wa kisiasa.

Matokeo rasmi ya uchaguzi wa Senegal yanatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa ambapo ikiwa hakutakuwa na mgombea aliyetimiza asilimia 50 ya kura zote uchaguzi huo utalazimika kwenda duru ya pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.