Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Hatua ya INEC ya kusogeza mbele uchaguzi Nigeria yaibua maswali mengi

Wananchi wa Nigeria wanaendelea kusibiri kupiga kura baada ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Februari 16 kuahirishwa hadi Jumamosi Februari 23, 2019.

Masanduku ya kura nchini Nigeria yamehifadhiwa baada ya tangazo la kusogeza mbele uchaguzi kwa wiki moja.
Masanduku ya kura nchini Nigeria yamehifadhiwa baada ya tangazo la kusogeza mbele uchaguzi kwa wiki moja. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria ilitangaza kuahirisha uchaguzi mkuu kwa juma moja, hatua iliyochukuliwa ikiwa ni saa chache tu zilikuwa zilisalia kabla ya wananchi wa taifa hilo kupiga kura.

Hatua hiyo ya Tume ya Uchaguzi INEC imewashangaza wengi na baadhi kutilia shaka iwapo uchaguzi huo utakuwa huru, wa kuaminika na wa wazi.

Jumla ya wagombea 73 wanawania kiti cha urais katika uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi inasema imefikia uamuzi wake baada ya kutafakari kwa kina kuhusu masuala ya usafirishaji wa vifaa na kufika kwa wakati kwenye vituo, changamoto ambayo tume hiyo inasema isingewezekana kuwa na uchaguzi huru, haki na wakuaminika.

Hata hivyo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, INEC, Mahmood Yakubu, akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia siku ya upigaji kura, amesema kwa ratiba ilivyo, isingewezekana tena kwa uchaguzi huo kufanyika kwa wakati.

Waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo wametoa wito kwa raia wa taifa hilo kuwa watulivu wakati maandalizi ya uchaguzi yanaendelea.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Mahmood Yakubu, amedai kuwa kuchelewa kwa uchaguzi huo hakuhusiani na ushawishi wa kisiasa kwa namna yeyote.

Wagombea mbalimbali katika kiti cha urais ikiwa ni pamoja na rais anaye maliza muda wake Muhammadu Buhari na mpinzani wake Atiku Abubakar wameelezea kutoridhishwa kwao na hatua hiyo ya tume ya uchaguzi kusogeza mbele tarehe ya upigaji kura kwa madai ya kutokamiliaka kwa baadhi ya maandalizi muhimu.

Rais Muhammadu Buhari anawania kuchaguliwa kwa muhula wa pili lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa kiongozi mkuu wa upinzani na makamu wa rais wa zamani, Atiku Abubakar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.