Pata taarifa kuu
AU-AL SISI-PAUL KAGAME

Al Sisi akabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU)

Vongozi wa Umoja wa Afrika wanakutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, kujadili masuala mbalimbali kuhusu biashara na usalama na wakati uo huo, rais wa Misri Abdel Fatta al Sisi amekuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja huo.

Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, rais wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi
Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, rais wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi Al Jazeera
Matangazo ya kibiashara

Al Sisi anamrithi rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu wa mwaka mmoja.

Rais Kagame amekabidhi Unyekiti wa Umoja huo katika mkutano mkuu wa 32 wa siku mbili, ulioanza leo.

Wkaati wa uongozi wake, rais Sissi anatarajiwa kushughulikia masuala ya usalama lakini pia kuongoza mageuzi ya fedha miongoni mwa nchi wanachama.

Mbali na suala hili, kiongozi huyo wa Misri anatarajiwa kutoa uongozi kuhusu namna ya kushughulikia tatizo la wahamiaji haramu wanaotoka mataifa ya Afrika, kwenda barani Ulaya na kwa bahati mbaya kuzama baharini.

Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International, imekosoa rais wa Misri kukabidhiwa nafasi hiyo kwa sababu ya kile wanachosema ni rekodi mbaya ya haki za binadamu nchini mwake.

Mbali na Unyekiti wa Umoja huo, viongzi hao pia wanajadiliana kuhusu masuala ya biashara miongoni mwa mengine yanayoliathiri bara la Afrika.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi ahutubia mkutano wa AU kwa mara ya kwanza

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Thisekedi, amehotubia mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa.

Imekuwa ni hotuba yake ya kwanza, kwa viongozi wenzake.

Tshisekedi amesema, mabadiliko ya amani ya madaraka yaliyofanyika nchini mwake, baada ya rais wa zamani kukabidhi madarakani, imeonesha kuwa DRC imekuwa kisiasa.

Rais huyo ambaye yupo Addis Ababa, baada ya ziara nchini Congo, Angola na nchini Kenya amesema hatua iliyofikiwa nchini mwake itasaidia sana katika uimarishwaji wa amani na uongozi wa sheria.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.