Pata taarifa kuu
DRC-UN-FAYULU-SIASA

DRC: Martin Fayulu akosoa kauli ya Antonio Guterres

Pamoja na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi nchini DRC, siku ya Jumatano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na utawala mpya nchini humo.

Kiongozi wa upinzani DRC, Martin Fayulu, Desemba 20, 2018 Kinshasa
Kiongozi wa upinzani DRC, Martin Fayulu, Desemba 20, 2018 Kinshasa © REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Antonio Guterres ametaka kuepo na serikali itakayo undwa na pande zote husika katika siasa ya DRC, kwa kuunganisha raia wote wa nchi hiyo.

Kwa upande wa kiongozi wa upinzani Martin Fayulu, ambaye bado anadai kile anachosema "ukweli wa uchaguzi", amesema Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kufuatana na mwenendo au msimamo wao kuna hatari wapotoshe wananchi wa DRC kwa kupindisha demokrasia na kuweka mbele maelewano ya kisiasa.

Naona kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hajasahau kilichotokea nchini DRC, yaani, mapinduzi ya uchaguzi. Lakini muono wangu ni kana kwamba DRC ni chi tofauti na kile kinachotokea nchini Venezuela kwa mfano, ambapo jumuiya ya kimataifa inaonekana kutoa shinikizo kwa utawala wa nchi hiyo kwa kufanyika uchaguzi mpya.

"Tatizo leo ni kuwakubalisha wananchi wa DRC, na ulimwengu mzima, kwamba mtu aliye pata 17% ya kura ndiye anayepaswa kuwa rais wa nchi, na yule aliyepata zaidi ya 62% ameshindwa uchaguzi. Ikiwa jumuiya ya kimataifa inataka kudidimiza demokrasia nchini KDRC, watwambie, kwani nani kesho atakuwa tena na imani na uchaguzi ?, " Martin Fayulu, amesema akihojiwa na RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.