Pata taarifa kuu
MISRI-SIASA-USALAMA

Katiba kufanyiwa marekebisho kumuwezesha Sissi kuwania muhala mwengine

Wabunge zaidi ya mia moja nchini Misri wamewasilisha rasimu ya marekebisho ya Katiba kumruhusu Rais Abdel Fattah al-Sissi kuwania muhula mwengine katika uchaguzi wa urais baada ya muhula wake wa pili kumalizika mwaka 2022, kwa mujibu wa vyanzo kutoka bungeni.

Picha za Rais Abdel Fattah al-Sisi huwekwa kila mahali. Cairo, Januari 22, 2018.
Picha za Rais Abdel Fattah al-Sisi huwekwa kila mahali. Cairo, Januari 22, 2018. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Nakala hiyo,iliyowasilishwa kwa Spika wa bunge Ali Abdel Aal, inaomba marekebisho kadhaa kwenye Katiba, ikiwa ni pamoja na moja ambayo inataka muhula wa rais uongezwe kutoka miaka minne hadi mikaa 6.

Katiba ya sasa inamruhusu rais kuwania kwa mihula miwili tu.

Ikiwa marekebisho hayo yatapitishwa Bw Sissi anaweza kuwania mara mbili katika uchaguzi wa urais baada ya mwaka 2022.

Bw Abdel Aal amepokea ombi kutoka kwa wabunge 120 kwa jumla ya 596 kurekebisha baadhi ya Ibara za Katiba, sawa na idadi inayohitajika kwa kupitisha rasmu hiyo, kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa bunge la Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.