Pata taarifa kuu
CAR-MAZUNGUMZO-USALAMA

CAR: Sherehe ya kutiwa saini kwenye mkataba wa amani yaahirishwa

Sherehe iliyokuwa imepangwa kufanyika Jumapili katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kuhusu makubaliano ya amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imeahirishwa.

Jean-Pierre Lacroix (kushoto) Mkuu wa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa na Smaïl Chergui (katikati), kamishna wa amani na usalama wa Umoja wa Afrika wakati wa mazungumzo huko Khartoum.
Jean-Pierre Lacroix (kushoto) Mkuu wa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa na Smaïl Chergui (katikati), kamishna wa amani na usalama wa Umoja wa Afrika wakati wa mazungumzo huko Khartoum. ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makundi 14 ya waasi yaliyowakilishwa katika mazungumzo na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yalitarajia kutia saini kwenye mkataba walioafikiana Jumamosi wiki hii iliyopita.

Hata hivyo makundi yote yameelezea furaha yao baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo mjini Khartoum.

Baada ya siku kumi ya mazungumzo, siku ya Jumamosi Umoja wa Afrika ulitangaza kwamba makundi ya waasi na Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefikia makubaliano. Kila upande umeridhia, lakini bila kutoa maelezo.

Makundi ya watu wenye silaha yanadhibiti karibu asilimia 80 ya nchi hiyo , makubaliano haya mapya - ambayo ni ya nane sasa- yameleta matumaini mapya kwa wananchi wa taifa hilo, hata kama kwa sasa hayajawekwa wazi.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, mkataba huo unazungumzia masuala nyeti kama msamaha kwa makundi ya waasi, kuundwa kwa serikali ya umoja, wapoganaji kutoka makundi mbalimbali kuingizwa katika vikosi vya usalama na ulinziu, na kutafutia suluhu matatizo mengine yanayuikabili nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.