rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Somalia Al Shabab Ugaidi

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu wawili wapoteza maisha mjini Mogadishu

media
Shambulizi la bomu mjini Mogadishu REUTERS/Feisal Omar

Watu wawili wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa baada ya gari lililokuwa na vilipuzi kulipuka karibu na Ofisi za Wizara ya mafuta mjini Mogadishu nchini Somalia.


Mohamed Abdullahi Tulah, afisa wa usalama nchini humo. amesema gari hilo lilikuwa limeegeshwa karibu na kituo cha mafuta wakati  lilipolipuka siku ya Jumanne mchana.

Mwanamke aliyekuwa anauza chai karibu na kituo hicho cha mafuta, ni miongoni mwa watu wawili waliopoteza maisha.

Hakuna kundi lililodai kutekeleza shambulizi hilo.

Hata hivyo, magaidi wa Al Shabab ambao wanaipinga serikali ya Mogadishu wamekuwa wakishiriki katika mashambulizi kama haya kulenga maafisa wa serikali.

Licha ya kuondolewa kutoka mji huyo, Al Shabab linasalia kundi hatari kwa usalama wa mji na nchi hiyo.