Pata taarifa kuu
MACRON-AL SISI-UFARANSA-MISRI

Rais Macron ashtumu hali mbaya ya haki za binadamu nchini Misri

Rais wa Ufaransa Emmaniel Macron ameshtumu kuongezeka kwa visa vay ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Misri katika uongozi wa rais Abdul-Fattah al-Sisi, ikilinganishwa na serikali zilizopita.

Rais wa Misri Fatah  al-Sisi akisalimiana na mgeni wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Januari 28 2019
Rais wa Misri Fatah al-Sisi akisalimiana na mgeni wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Januari 28 2019 AFP / Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Macron akiwa jijini Cairo, baada ya mazungumzo na mwenyeji wake,  kiongozi huyo wa Ufaransa amesema rekodi ya haki za binadamu katika taifa hilo la Afrika Kaskazini ni mbaya sana na licha ya kuwa mshirika wa karibu wa Misri, uongozi uliopo unastahili kuangazia suala hili.

Kauli hii ya rais Macron hata hivyo, imepingwa vikali na rais al-Sisi, amesema haki lazima zizingatie usalama na vita dhidi ya ugaidi nchini humo na kumwambia mgeni wake kuacha kuangazia suala hili kwa macho ya nchi za Magharibi.

“Uthabiti wa jamii unategemea sana na namna jamii ilivyo uthabiti na amani ya muda mrefu, unakwenda sambamba na kuheshimu ghaki za binadamu na sheria,,” amesema rais Macron.

“Naiheshimu Misri lakini katika hili, ni lazima tuendelee kulizungumzia hili,” ameongeza.

Mbali na suala hilo, viongozi wa mataiufa hayo mawili wametia saini mikataba kadhaa ili kuendelea kushirikiana katika masuala ya usalama na biashara kati ya Paris na Cairo.

Misri ambaye ni mshirika wa karibu wa Ufaransa, inategemea taifa hilo la bara Ulaya kuhusu ununuzi wa silaha.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.